Friday, August 22, 2008

KARIBUNI SANA!!

Ndugu wa-Tanzania na watu wote nawakaribisha sana katika blog yetu hii mpya.Blog hii imeanzishwa kwa ajili ya kuangalia matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii yetu ikiwepo Umasikini,Magonjwa,Kukosa elimu na mengine mengi..ikiwepo makazi,chakula,mavazi na mengine mengi.. Tuangalie jinsi ya kusaidia kutatua matatizo hayo kwa hali na mali ikiwepo kusaidiana kimawazo!!
Tunakaribisha makampuni,mashirika na hata watu binafsi watakaokua tayari kuidhamini hii blog ili kuwafuata wanajamii huko waliko na kujua matatizo yao na jinsi ya kuyaleta kwenye blog ili jamii iweze kuwasaidia ikiwepo pia mfuko wa blog utakaochangiwa na walioguswa na matatizo ya hao watu pamoja na wadhamini wa hii blog.

ninaamini tutaweza kuwafikia wanajamii wenye matatizo na kuongea nao na kuangalia jinsi ya kuwasaidia na pia kuleta picha zao na maelezo yao yote....

Wanajamii hebu tuunganishe nguvu zetu katika swala hili ili tumsaidie Mtanzania yule anayekumbwa na matatizo na ninaamini tutakuwa na jamii imara na mungu ataendelea kutusaidia na kutubariki...
Asanteni
Jamiiyetu Team!!